Hit enter to search or ESC to close
Tanzania
ENGIE Energy Access

Tanzania

ENGIE Energy Access Tanzania inatoa huduma za mitambo ya umeme wa jua yenye uwezo wa kuwasha taa, kuchaji simu, runinga, redio na kadhalika. Malipo ni ya mfumo rahisi kabisa wa kulipia kwa awamu kupitia mitandao ya simu (Vodacom, Airtel, Tigo au Halotel). Tunawawezesha wale wanaotafuta nishati safi, wasio kwenye gridi ya taifa kupata umeme na mikopo mingine yenye manufa katika maisha ya wateja wetu.

Pamoja tuna nguvu zaidi

Huduma zetu Tanzania zilianza mnamo mwaka 2013 kwa jina Mobisol Tanzania na tangu hapo tumenufaisha zaidi ya wateja 125,000 kupitia nishati yetu safi, na kufikia maisha ya Watanzania zaidi ya laki sita na nusu.

Mnamo mwaka 2020, ENGIE Group ilitukutanisha na Fenix International na ENGIE PowerCorner kuunda ENGIE Energy Access. Pamoja tuna nguvu zaidi na tunazidi kukua kote Afrika pindi tunapojiandaa kuzindua jina letu jipya MySol.

Kwa sasa tuna zaidi ya wafanyikazi 250 na maduka zaidi ya 40 kote nchini. Timu yetu ya Tanzania Imeji kutoa huduma ya kipekee kwa wateja. Bidhaa zetu zenye ubora wa hali ya juu (zilizoundwa Marekani na Ujerumani) zina hakikisha wateja wetu ni wenye furaha muda wote.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

MYSOL ni jina jipya la brand ambalo litachukua nafasi ya kile kinachojulikana leo kama Fenix au Mobisol.

Kufuatia muungano wa Fenix International, Mobisol na PowerCorner kuunda ENGIE Energy Access, kampuni imejenga wigo mpana zaidi wa bidhaa mbalimbali kwa kuleta pamoja bidhaa kutoka Fenix na Mobisol.

MYSOL inaendelea kukupa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu unazozijua na kuziamini.

Mara tu unapoamua kununua mtambo wa sola, timu yetu ya mauzo itachukua taarifa zako za mawasiliano.

Baada ya hapo utapokea simu ya tathmini ya mteja kwa kwa ajili ya uthibitisho wa uwezo wako wa kuulipia mtambo unaohitaji kununua

Malipo hufanywa kwa urahisi kwa njia ya simu kupitia Vodacom, Airtel, Tigo au Halotel.

Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi: Tunaelewa kuwa kuna wakati ambapo changamoto za kifedha zinaweza kutokea

Tutawasiliana nawe kuelewa changamoto yako na kukushauri ipasavyo ili kukubaliana namna ya kudhibiti mpango wa malipo.

Ndio! Utakuwa ni mmiliki kamili mwenye uhuru wa mtambo wako wa sola baada ya kumaliza malipo yako yote ya mkopo.

Ikiwa mtambo wako haufanyi kazi, unaweza piga simu kwa huduma kwa wateja BURE kupitia 0800 755 000 kwa msaada”

Ikiwa tatizo katika mtambo wako haliwezi kutatuliwa kupitia maongezi ya simu, tutapanga moja ya mafundi wetu afike nyumbani kwako, atambue tatizo, na kisha kulitatua hapo hapo nyumbani kwako na kukupatia ushauri kuhusu marekebisho yeyote ya muhimu.

Ndio! mitambo yetu inakuwezesha kupata kipato cha ziada. Kwa mfano, kuwachajia simu wanao kuzunguka au kuonyesha mechi za mpira kwa kutumia runinga yetu kubwa ya sola.

Pia tunawazawadia kati ya Tshs 41,000 hadi Tshs 104,000 wateja wetu wanaopendekeza/shauri ndugu, jamaa, na marafiki kununua na kumiliki mitambo yetu ya sola.

Mteja yeyote atakayenunua mtambo wetu kutokana na ushawishi na ushauri wako, basi utajipatia kati ya Tshs 41,000 hadi Tshs 104,000

Ndio ni rahisi

Wasiliana nasi kwa kutumia namba yetu ya bure au wakala wetu yeyote wa mauzo.

Tutapitia tarifa zako za kipato kujua kama unafuzu kupata mtambo mkubwa zaidi.

Baada ya kufuzu, utalipa ada ya kubadilisha mtambo ya Tzh 65,000 na kianzio kilichopunguzwa.

Nenda kwenye duka letu lolote lilipo karibu yako ili upate mkataba mpya na ukabidhiwe mtambo wako

Namba ya huduma kwa wateja na mahali maduka yetu yanapatikana

Namba ya huduma kwa wateja na mahali maduka yetu yanapatikana

Ili kununua bidhaa yetu yeyote piga 0800 755 000 BURE

au tembelea duka letu la karibu

Jiunge na familia ya ENGIE Energy Access! #TimuMoja

Jiunge nasi katika dhamira yetu ya kuboresha maisha Afrika na suluhisho la nishati safi ya jua, nafuu na bunifu.

Jiunge na familia ya ENGIE Energy Access! #TimuMoja

Makao Makuu Tanzania

ENGIE Energy Access - Tanzania

Plot Taso/G/448

Nane Nane Grounds, Arusha

Tanzania